Owoh alikuwa kati ya waigizaji wakuu katika filamu ya 2003 ya Osuofia i London . Anajulikana pia kwa kuuimba wimbo wa I Go Chop Your Dollar, unaohusu ufisadi wa ada ya mapema. Wimbo huu ulitumika katika filamu ya The Master ambapo Owoh hucheza kama mtapeli.[2] Tume ya Uhalifu wa Fedha na Uchumi na Tume ya Utangazaji ya Nigeria ilipiga marufuku wimbo huo[3]. Mwaka 2007 alikamatwa na polisi mjini Amsterdam, Uholanzi(kitongoji Bijlmermeer katika eneo la Amsterdam Zuidoost) kama matokeo ya uchunguzi wa miezi 7 ulioitwa "Operation Apollo".[2] Owoh alikuwa akitumbuiza wakati polisi walivamia pahali pale na kuwatia mbaroni watu 111 kwa tuhuma za udanganyifu makosa ya uhamiaji. Owoh baadaye aliachiliwa huru.[3][4] Mwezi Novemba 2009, Owoh alitekwa nyara eneo la mashariki mwa Nigera. Wateka nyara walitaka naira milioni 15 kama makombozi. Aliachiliwa huru baada ya familia yake kutoa naira milioni 1.4 kama makombozi.